One of the participants during the Musabaqah Semi Finals

Siku mbili za Jumanne na Jumatano, Septemba 8 na 9, 2020, yalifanyika mashindano ya watu wazima ya Nusu Fainali ya Qur’ani Tukufu nchini Brunei. Mashindano hayo ya siku mbili yaliyofanyika katika Ukumbi wa Melor wa Wizara ya Masuala ya Dini ya Brunei (MoRA) yalianza Jumanne ya tarehe 8 Septemba, 2020 na kurushwa moja kwa moja hewani. Washiriki 23 walichuana kwenye siku ya kwanza ya mashindano hayo huku wakichunga protokali zote za afya kwa ajili ya kuepusha maambukizo ya COVID-19.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Qur’ani nchini Brunei

Washiriki 18 waliosalia walichuana siku ya pili yake ya Jumatano, Septemba 9, 2020, mashindano ambayo yalirushwa hewani mubashara katika mitandao ya kijamii.

Mashindano hayo ya Nusu Fainali ya Qur’ani Tukufu katika kategoria za Qiraa na Hifdh yalilenga kulea wataalamu zaidi wa Qur’ani katika jamii ya nchi hiiyo ili kuimarisha ukuruba wao kwa Kitabu hicho kitakatifu na kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema. Shabaha nyingine ya mashindano hayo yaliyowashirikisha maqarii wa kike na wa kiume ni kushajiisha usomaji wa Qur’ani kwa makhraj nzuri, kwa sauti ya kuvutia na kujenga utamaduni wa kuitanguliza mbele Qur’ani Tukufu katika jamii.

(Visited 44 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!