Wizara ya Wakfu ya Oman imetangaza habari ya kuanza kufanya kazi mfumo maalumu wa elektroniki kwa ajili ya kutoa huduma zinazohusiana na misikiti na kurahisisha kuitambua misikiti na maeneo ya Sala nchini humo.

Hayo yameripotiwa na mtandao wa “khabrna” ambao umeinukuu Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Oman ikitangaza habari hiyo na kusema kuwa, lengo la mfumo huo wa elektroniki ni kutoa huduma kamili zinazohusiana na misikiti na maeneo ya Sala nchini Oman.

Namna unavyofanya kazi mfumo huo

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mfumo huo utakuwa unatoa nambari maalumu kwa watumiaji wake kuhusiana na maeneo hayo ya ibada.

Huduma zake

Ikitoa ufafanuzi zaidi, Wizara ya Wakfu ya Oman imesema, mfumo huo wa elektroniki umeundwa katika maeneo manne makuu ya utumiaji, na ndani yake mnatolewa huduma 21 za elektoroniki.

Maelezo mbalimbali kuhusu misikiti, historia zake, hatua ilizopitia n.k, ni miongoni mwa maelezo ambayo watumiaji wa mfumo huo wataweza kuyapata kupitia nambari maalumu zitakazokuwa zinatolewa.

Umuhimu wa Mfumo wa Elktroniki wa Misikiti ya Oman

Wizara ya Wakfu ya Oman imesema kuwa, imekusudia kuufanya bora mfumo huo kiasi kwamba uwe na uwezo wa kuorodhesha taarifa za misikiti yote mikuu ya nchi hiyo kwa njia ya otomatiki. Mfumo huo umeanzishwa kama sehemu ya mpango wa taifa wa Oman wa kujua idadi ya misikiti mikuu na midogo na maeneo ya Sala. Vile vile una lengo la kuiwezesha Wizara ya Wakfu ya Oman kutoa huduma kwa njia bora zaidi katika maeneo hayo ya ibada.

Mfumo huo utatoa elimu kuhusu idadi ya misikiti na maeneo ya Sala, sehemu ilipo, historia, kumuwezesha mtu kujua ulipo msikiti wa karibu na eneo alipo yeye wakati huo bila ya kuuliza wenyeji wa eneo hilo. Watumiaji wanaweza kujiunga na mfumo huo kupitia nambari ya uraia, nambari ya utaifa au nambari ya simu.

(Visited 55 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!