Mmiliki bora wa Benki za Kiislamu kwa mwaka huu wa 2020 amechaguliwa katika eneo la Mashariki Kati.
Mtandao wa habari wa “PK Obsever” umesema kuwa Meneja Mkuu wa Qatar Islamic Bank (QIB), Bw. Bassel Gamal amechaguliwa kuwa mmiliki bora wa benki za Kiislamu katika sherehe za Tunzo za Fedha za Kiislamu (Islamic Finance Awards) kwa mwaka huu wa 2020.
Mwaka 2013 Gamal alichukua jukumu la kuongoza kitengo cha mabadiliko ya kiistratijia cha Benki ya Kiislamu ya Qatar na ametoa mchango mkubwa katika mafanikio ya benki hiyo ya kuimarisha biashara, kuleta mapinduzi ya kidijitali na kustawisha utamaduni wa biashara.
Bassel Gamal amechaguliwa pia kutwaa tunzo ya benki bora ya Qatar ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo ambapo Benki ya Kiislamu ya Qatar inachukua tunzo hiyo. Benki hiyo ni ya pili kwa ukubwa kati ya benki binafsi nchini humo. Benki ya Kiislamu ya Qatar iliasisiwa mwaka 1982 na mbali na Qatar ina matawi yake pia katika nchi za Sudan, Lebanon na Uingereza. Hivi sasa benki hiyo ina wafanyakazi zaidi ya elfu moja katika kila kona ya dunia.