Masjid al Rahman, ni Msikiti wa aina yake uliojengwa katikati ya mto kwenye kijiji cha Pulau Gajah, karibu na Kora Bharu, Kelantan, huko kaskazini mashariki mwa Malaysia.

Miongoni mwa vivutio vya aina yake vya utalii wa kidini nchini Malaysia ni Misikiti yake ya kuvutia ukiwemo huu Msikiti mkubwa uliozungukwa na maji kila sehemu.

Msikiti huo umetawaliwa na usanifu majengo wa Malay na hicho ni kivutio kingine kwa watu wa kila namna.

Eneo ulipojengwa Msikiti huo lenyewe lina mvuto wa kipekee wa kimaumbile, linapendeza sana na ni eneo tulivu lisilo na kelele.

Sensa ya mwaka 2010 inaonesha kuwa, asilimia 61.3 ya Waislamu wa Malaysia wanatekeleza na kuheshimu mafundisho ya dini yao.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari la AboutIslam, Uislamu uliwasili nchini Malaysia miaka 700 iliyopita. Hata hivyo miaka 400 ya uvamizi na ukoloni wa nchi za Ulaya ambao ulimalizika takriban nusu karne tu iliyopita yaani mwaka 1957 uliwafanya baadhi ya watu wasitekeleze inavyopasa mafundisho ya Uislamu huko Malaysia.

Pamoja na hayo, Uislamu umezidi kupata nguvu nchini Malaysia tangu baada ya kutimuliwa wakoloni wa Ulaya katika nchi hiyo ya Waislamu.

Hapa chini tumeweka kipande kifupi cha video kuhusu Msikiti huo.

(Visited 66 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!