Na Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali anayoiongoza itahakikisha inashirikiana vyema na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) katika kujenga misingi ya dini ya Kiislamu hapa nchini.
Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo (Jumatatu) wakati alipofanya mazungumzo na Wajumbe wa Jumuiya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) wakiongozwa na Kaimu Katibu Sheikh Ali Abdalla Amour Ikulu Jijini Zanzibar.
“Dk. Hussein Mwinyi: Miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele katika kujenga misingi ya dini ya Kiislamu ni umoja, amani na mshikamano.”
Wajumbe wengine kutoka (JUMAZA) waliofika Ikulu kuzungumza na Rais ni Dk. Moh’d Hafidh Khalfan, Sheikh Masoud Hemed Nassor, Sheikh Yussuf Khamis, Sheikh Abdalla Issa Makame, Sheikh Muhiddin Zubeir Muhiddin na Ukhti Halima Qasim Moh’d.
Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Hussein Mwinyi amesema kuwa miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele katika kujenga misingi ya dini ya Kiislamu ni umoja, amani na mshikamano.