Skuli pekee iliyokuwa inaruhusu nembo za kidini mjini Paris Ufaransa imefungwa na serikali ya Emmanuel Macron ambaye ameshindwa kuficha chuki zake dhidi ya mafundisho ya dini na hasa Uislamu.

Gazetila Daily Sabah la nchini Uturuki limeripoti habari hiyo katika toleo lake la mtandaoni na kuongeza kuwa, Skuli ya Sekondari ya Meo ya mjini Paris Ufaransa imefungwa kwa madai ya “kukabiliana na misimamo mikali ya Kiislamu.”  Shule hiyo ni maarufu kwa kuruhusu wanafunzi wa dini zote kuingia shuleni hapo wakiwa na nembo za dini zao bila ya kubugudhiwa. Wanafunzi Waislamu, Wakristo, Mayahudi na wengineo walikuwa wanaendelea vyema na masomo yao bila ya matatizo yoyote katika shule hiyo.

Baada ya kufungwa skuli hiyo, sasa wanafunzi 110 wameachwa njia panda wakiwa katika katikati ya muhula wa masomo.

Mkuu wa shule hiyo, Hanane Loukili ameliambia shirika la habari la Anadolu kuwa, madai yaliyotolewa na serikali ya kwamba skuli hiyo inahamasisha watu kujitenga ni ya kipuuzi na hayana msingi wowote, bali sababu kuu ya kufungiwa shule yetu ni kwa kuwa tumetoa uhuru kwa wanafunzi wa dini zote kutekeleza mafundisho ya dini zao bila ya bugudha.

Shule hiyo imeamua kukata rufaa kupinga uamuzi huo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tangu mwezi Januari 2020 hadi hivi sasa skuli hiyo imekuwa ikisumbuliwa sana na maafisa wa serikali ya Emmanuel Macron ambao mara kwa mara wamekuwa wakifika shuleni hapo kufanya uchunguzi na ukaguzi kuhusu majengo au kazi za ofisini n.k.

Vile vile mkuu wa shule hiyo amesema, madai mengine ya viongozi wa Paris kuhusu walimu Waislamu wa skuli hiyo, pia hayana mashiko kwani walimu kutoka Algeria na Tunisia wamekuwa wakisomesha shuleni hapo bila ya matatizo yoyote, kazi zao ni halali na zinasimamiwa kikamilifu na mamlaka husika.

Pamoja na hayo, tarehe 9 Disemba, 2020, maafisa wa Wizara ya Mahakama na Jeshi la Polisi la Paris walisema mbele ya waandishi wa habari kwamba skuli hiyo itafungwa katika sehemu ya kile walichodai kuwa ni kupambana na eti “Uislamu wa misimamo mikali” na kwa ajili ya eti kuwalinda watoto na vijana. Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo, Hanane Loukili aidha amesema, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, shule hiyo imefuata sheria zote za kisekula zilizowekwa na serikali bali hakuna somo lolote la dini linalofundishwa shuleni hapo.

(Visited 73 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!