Timu ya Barcelona ya nchini Uhispania imewawekea wachezaji wake ratiba maalumu za kutekeleza mafundisho ya kidini na lishe kama sehemu ya kuuenzi na kuuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani na pia kuhakikisha kuwa wachezaji hao hawaumizwi na mazoezi magumu wakati wakiwa katika saumu.

Hayo yameripotiwa na mtandao wa “Mosaique FM” ambao umesema kuwa, timu ya mpira wa miguu ya Barcelona imewawekea ratiba maalumu ya lishe wachezaji wake Waislamu kwa mnasaba wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ili kuwapunguzia uzito wa kufanya mazoezi wakiwa wamefunga. Wachezaji watatu Waislamu wa Barcelona ambao ni Miralem Pjanić, Ousmane Dembélé na Ilaix Moriba (Moriba Kourouma Kourouma) wamewekewa ratiba maalumu ya kutekeleza ibada zao za kidini pamoja na chakula maalumu ili wasipate tabu katika mashindano na mazoezi wakiwa kwenye saumu.

Miongoni mwa ratiba hizo ni kuhakikisha kwanza wanapata nyama zilizochinjwa Kiislamu, kiwango cha maji hakipungui miilini mwao na hawaitumi kupindukia miili yao.

Wachezaji hao Waislamu wa timu ya Barcelona ya Uhispania wamewekewa kiwango maalumu cha kunywa vitu vya maji maji na chakula katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani, kiwango ambacho hakiwatii kwenye uzito wakati wa mashindano na mazoezi. Timu ya Barcelona imesajili wachezaji wengi Waislamu katika miaka ya hivi karibuni. Siku chache zilipita, timu hiyo ya Uhispania ilisambaza mkanda wa video unaotoa mkono wa baraka na wa kheri na fanaka kwa Waislamu duniani kwa mnasaba wa kuingia mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

(Visited 51 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!