Ukumbi wa tawaf (kutufu) wa Kibla cha Waislamu AlKaaba katika Msikiti Mtakatifu wa Makkah umevunja rekodi ya kuoshwa wote kwa muda mfupi wa dakika 5 tu katika siku ya pili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Watu 4,000 wameshiriki katika usafi huo na kufanikiwa kuweka rekodi hiyo.

Shirika la habari la Saudi Arabia limeripoti kuwa, kitengo cha usafi na kutandika mabusati cha Masjidul Haram (Msikiti Mtukufu wa Makkah) kilichoko chini ya Idara Kuu ya Masuala ya Msikiti wa Makkah na Msikiti wa Mtume Madina ndicho kilichofanya usafi huo katika muda mchache kabisa kuwahi kufanyika zoezi hilo.

Maafisa wa idara hiyo wamesema kuwa, zoezi hilo la usafi limefanyika katika kipindi kifupi zaidi cha dakika 5 na hiyo ni rekodi mpya ya usafi katika eneo hilo takatifu.

Jaber Wud’ani (?) Mkuu wa Idara ya Usafi ya Masjid al Haram amesema kuwa, tani 291 za taka zimekusanywa katika dakika hizo 5 za usafi wa ukumbi wa kutufu wa AlKaaba.

Aidha amesema: Wafanyakazi 4,000 wameshiriki katika zoezi hilo. Zaidi ya hayo, malori 1,500 ya taka na mapipa 1,5000 madogo madogo yametumika katika usafi huo.

Hapa chini tumeweka kipande kifupi cha video cha zoezi hilo:

One thought on “Video: Ukumbi wa AlKaaba wavunja rekodi ya kuoshwa wote kwa dakika 5”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!