Watu wasiojulikana wenye silaha wameuawa watu 13 katika vijiji viwili vya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraisa ya Congo.
Shirika la habari la Reuters limenukuu duru za kijeshi za DRC na kusema kuwa, mashambulizi hayo ni ya karibuni kabisa kutokea nchini humo na yamefanywa na waasi wa ADF-Nalu. Umoja wa Mataifa unasema mauaji hayo yanaweza kuhesabiwa kuwa ni jinai ya kivita.
Taarifa zinasema kuwa mauaji hayo yametokea katika mkoa wa Kivu Kaskazini wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo tangu mwaka 2019 hadi hivi sasa zaidi ya raia 1,000 wameshauawa katika mashambulio kama hayo. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, waasi hao waliwafunga pingu wakazi wa vijiji viwili vya Kinziki-Matiba na Wikeno kabla ya kuwaua Ijumaa jioni.