Vyombo vya habari vya Marekani vimetangaza kuwa, mshauri mmoja wa zamani wa ngazi za juu wa rais wa Marekani, Donald Trump ametiwa mbaroni kwa utapeli na udanganyifu.

Waendesha mashtaka wa serikali ya shirikisho ya Marekani, wamemtia mbaroni Stephen Bannon, mwanastratijia wa ngazi za juu wa zamani wa Ikulu ya Marekani, White House na maafisa wengine watatu.

Waendesha mashtaka hao wamesema mjini New York kwamba Bannon ametiwa mbaroni kwa shutuma za kufanya utapeli wa mamia ya maelefu ya dola, pesa za watu wanaotoa misaada ya kifedha.

Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari, lengo la utapeli uliofanywa na mshauri huyo wa Donald Trump, ilikuwa ni kutafuta fedha za kusaidia mpango wa rais huyo wa Marekani wa kujenga ukuta katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico.

(Visited 21 times, 1 visits today)
One thought on “Mshauri wa zamani wa Trump atiwa mbaroni kwa utapeli”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!