Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umeamua kuipatia Lebanon msaada wa chakula wa tani 50 elfu baada ya silo pekee kubwa ya nchi hiyo kuteketea kikamilifu katika mripuko mkubwa uliotokea kwenye bandari ya Beirut.

Jumanne tarehe 11 Agosti 2020, Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa WFP ulitangaza kuwa umeamua kuipatia Lebanon msaada wa tani 50 elfu za unga wa ngano ili kuhakikisha nchi hiyo haikumbwi na upungufu wa bidhaa hiyo muhimu baada ya silo pekee ya kuhifadhia ngano kuteketea katika mripuko mkubwa wa Beirut.

Kwa mujibu wa idara ya uratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa akiba iliyopo ya unga inakidhi haja ya wiki sita za soko la Lebanon.

Shehena ya kwanza ya msaada huo itakuwa na tani 17 elfu na 500 za unga wa ngano na itafika Lebanon katika kipindi cha siku 10 zijazo kwa ajili ya kudhamini mahitaji ya mwezi mmoja ya nchi hiyo.

Jumanne jioni, tarehe 4 Agosti 2020, kulitokea moto mkubwa katika moja ya maghala ya kuhifadhia mada za miripuko kwenye bandari ya Beirut. Baada ya hapo kulirtokea mripuko mkubwa katika ghala la pembeni lililokuwa na tani elfu mbili za mada za ammonium nitrate. Hadi hivi sasa zaidi ya watu 160 wameshauawa na karibu elfu sita wengine wamejeruhiwa kutokana na janga hilo.

(Visited 98 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!