Taasisi mbalimbali Kiislamu nchini Marekani zimeitaka serikali ya nchi hiyo kuwa na mjumbe maalumu wa serikali kwa ajili ya kufuatilia na kukabiliana na chuki na propaganda chafu Waislamu.

Hayo yameripotiwa na USA Today ambayo imeongeza kuwa, Waislamu wa Marekani wamemwandikia barua rasmi rais wa nchi hiyo, Joe Biden wakimtaka atekeleze ahadi zake za kupambana na dhulma wanayofanyiwa Waislamu na ateue mwakilishi maalumu wa serikali ya kukabiliana na propaganda chafu zinazoenezwa nchini Marekani dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Katika barua yao hiyo, Waislamu wa Mambo wamesema, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya nchi hyo inaweza kusaidia juhudi za kupata suluhisho la tatizo hilo ambalo limeikaba kooni jamii ya Waislamu nchini Marekani. 

Wiki iliyopita Joe Biden alikiri katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwamba Waislamu wananyimwa haki zao, wananyanyaswa na kubughudhiwa katika jamii ya Marekani.

Chuki dhidi ya Waislamu ziliongezeka mno wakati wa uraia wa Donald Trump ambaye alikuwa hafichi chuki zake dhidi ya Waislamu. Maudhi unyanyasaji na mateso waliyopata Waislamu wakati wa utawala wa Donald Trump huko Marekani haujawahi kutokea mfano wake katika historia ya Marekani.

(Visited 16 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!