Waziri na balozi wa zamani wa Senegal amewarejeshea Wafaransa nishani yao waliyowahi kumpa, ikiwa ni sehemu ya kuonesha kukerwa kwake mno na vitendo vya kumvunjia heshima Nabii wa rehema, Mtume Muhammad SAW vilivyofanywa na gazeti la Charlie Hebdo la Ufaransa na kuungwa mkono na rais na viongozi wa Ufaransa.

Mtandao wa habari wa “Arabi 21” ameripoti habari hiyo na kusema kuwa, Balozi Amadou Tijan, waziri wa zamani wa utamaduni wa Senegal amemwandikia barua rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, na kumueleza kwamba haoni fakhari yoyote kuendelea kuwa na nishani ya fakhari ya Ufaransa kutokana na nchi hiyo ya Ulaya kumvunjia heshima Mtume Muhammad na matukufu ya Waislamu hivyo anawarejeshea wenyewe Wafaransa nishani yao hiyo. Ufaransa imempa nishani hiyo pia, Samuel Paty mwalimu Mfaransa aliyemtukana na kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.

Vile vile soma:

Maandamano, ususiaji wa Waislamu, wampigisha magoti Macron?

Waziri wa Ufaransa kutembelea al Azhar leo ili kupungua hasira za Waislamu

Tijan alikuwa balozi wa Senegal nchini Canada kwa miaka mingi. Amesema katika barua yake hiyo kwamba, wakati Wafaransa walipompa medali hiyo, alifurahi na kuona fakhari, lakini haona sababu yoyote ya kuendelea kukaa na medali hiyo ambayo amepewa pia aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.

Maandamano dhidi ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Vile vile amemshutumu rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwa kufanya njama za kuwageuza watu wapuuzi kuwa mashujaa wa taifa na kuongeza kwamba, awali nilikuwa nikidhani kwamba medali hii ni nembo ya udugu, uhuru na usawa lakini sasa nairejesha kwa ubalozi wa Ufaransa mjini Dakar, kulalamikia kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW huko Ufaransa. Kumlinda na kumuhami Mtume wa Uislamu ni fakhari kubwa zaidi kwangu kwani kila siku Waislamu wanatamka shahada mbili za kukiri kwamba hakuna mungu ila Allah na Muhammad ni Mtume wa Allah.

Gazeti la Charlie Hebdo la maadui wa Uislamu huko Ufaransa, lilichapisha tena vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammmad SAW mwezi uliopita. Rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron, aliunga mkono uhalifu huo na kuuita eti ni uhuru wa kujieleza. Uadui huo wa Wafaransa kwa Mtume Muhammad SAW na matukufu ya Uislamu yameamsha hasira kubwa za Waislamu kote ulimwenguni. Waislamu wa nchi mbalimbali wamesusia bidhaa za Ufaransa, hatua ambayo imewatia hofu kubwa viongozi wa dola hilo la kikoloni na kumfanya hata Emmanuel Macron adai kwamba amenukuliwa vibaya.

(Visited 16 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!