Mwezi wa kuwazindua watu kuhusu hatari za kueneza chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza, huadhimishwa mwezi Novemba kila mwaka kwa ajili ya kuwaelimisha watu kuhusu Uislamu na kufuta fikra potofu kuhusiana na Waislamu nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa “About Islam” kila mwaka kuna zaidi ya vitendo 7000 vya uhalifu unaotokana na chuki dhidi ya Waislamu vinatokea nchini Uingereza. Sasa kampeni ya mwezi Novemba imeanzishwa kwa makusudi ili kutangaza mchango mkubwa wa Waislamu nchini Uingereza na kuwazindua watu kuhusu madhara ya kueneza fikra za chuki dhidi ya Waislamu.

Kampeni ya mwezi huo wa Novemba imepewa jina la “Islamophobia Awareness Month” na inaendeshwa na Taasisi ya Ushirikiano na Ustawi wa Kiislamu (MEND) kwa kushirikiana na taasisi nyingine huko Uingereza. Kampeni hiyo ilianza mwaka 2012 kwa ajili ya kupambana na changamoto za kila namna wanazokumbana nazo Waislamu nchini humo.

Kaulimbiu ya kampeni ya mwaka huu ni “Mizizi ya Ubaguzi wa Rangi.” Katika kampeni ya mwaka huu, uenezaji wa chuki dhidi ya Uislamu umetajwa kuwa ni aina mojawapo ya ubaguzi wa rangi ambao unashambulia moja kwa moja itikadi na utekelezaji wa mafundisho ya dini hii.

(Visited 60 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!