Idadi ya maambukizo ya kirusi cha corona inazidi kuwa kubwa barani Afrika licha ya serikali za nchi mbalimbali barani humo kuanza kufungua sekta zao za kiuchumi baada ya miezi kadhaa ya kufungwa takriban kikamilifu shughuli hizo.

Kwa mujibu wa takwimu za karibuni kabisa kutoka kwa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kupambana na Magonjwa, bara hilo limeshathibitisha kesi 1,047,218 za wagonjwa wa corona ambapo hadi kufikia leo Jumatatu, idadi ya watu waliofariki dunia kwa ugonjwa huo barani Afrika ilikuwa imeshafikia 23,253.

Afrika Kusini imeendelea kuwa nchi iliyoathiriwa vibaya zaidi ya ugonjwa wa COVID-19 barani Afrika. Hadi hivi sasa nchi hiyo imesharekodi wagonjwa laki tano na 59,859 na tayari watu 10,408 wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa huo huko Afrika Kusini pekee.

Ukitoa Afrika Kuisni na Misri, nchi za Nigeria, (wagonjwa 46,577), Ghana, (wagonjwa 41,003), ndizo nchi zinazofuatia kwa kuwa na wagonjwa wengi zaidi wa corona barani Afrika.

Pamoja na hayo kuna habari pia za kutia moyo. Kwa mujibu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kupambana na Magonjwa, hadi hivi sasa wagonjwa laki saba na 33,375 wameshapona corona Afrika ambayo ni sawa na asilimia 70 ya wagonjwa wote.

(Visited 17 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!