Polisi nchini Ufaransa wamemtia mbaroni Rasmus Paludan, raia wa Denmark mwenye chuki na Uislamu na Waislamu ambaye pia ni mkuu wa chama cha Stram Kurs chenye misimamo mikali. Paludan amekwenda Paris Ufaransa kwa ajili ya kuchoma moto msahafu.

Kwa mujibu wa “al Quds al Arabi,” polisi wa Ufaransa wamemtia mbaroni adui huyo mkubwa wa Uislamu ambaye mara kwa mara anavunjia heshima matukufu ya Kiislamu, kabla hajafanya maandamano yaliyo dhidi ya dini tukufu Uislamu. Paludin alikuwa amepanga kufanya uhalifu huo katika eneo la Arc de Triomphe, katikati ya meidani ya Charles de Gaulle mjini Paris. Hata hivyo ametiwa mbaroni mara baada ya kukanyaga ardhi ya Ufaransa.

Katika upande mwingine, wakuu wa kieneo mjini Brussels Ubelgiji wamesema kuwa wamepiga marufuku adui huyo wa Uislamu kuingia mjini humo. Miezi michache iliyopita pia, maafisa wa polisi wa Sweden walipinga mpango wa mhalifu huyo wa kuchoma msahafu mbele ya msikiti katika moja ya miji ya kusini mwa nchi hiyo.

(Visited 13 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!