Sheikh Mahmoud Ibrahim Amir, ni mmoja wa wasomaji wenye sauti nzuri wa Qur’ani Tukufu raia wa Misri licha ya kwamba Mwenyezi Mungu amemnyima neema ya kuona.

Sheikh Amir ambaye pia amehifadhi Qur’ani nzima, alizaliwa mwaka 1987 katika kijiji cha Halawija cha wilaya ya Abu Matamir mkoani Buhayrah, Misri.

Alikuwa hajapindukia hata miaka mitano na nusu wakati alipojaaliwa kuhifadhi Qur’ani nzima. Alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani nzima katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi minne chini ya usimamizi na uangalizi wa Abu Zayd Bisyuni, mmoja wa wahadhiri wakubwa wa Qur’ani nchini Misri.

Mwenyewe Sheikh Mamdouh Amir anasema, alikuwa akihifadhi mistari 15 adhuhuri na mistari 15 alasiri kila siku. Anasema licha ya kwamba Mwenyezi Mungu amemnyima neema ya kuona, lakini amempa neema nyingine kubwa nayo ni uwezo wa kipekee wa kiakili wa kuhifadhi haraka aya za Qur’ani Tukufu na sauti nzuri ya kuvutia.

Mwaka huu wa 2020 qarii huyo kijana alialikwa nchini Afrika Kusini kusoma tajwidi na alisoma Qur’ani kwa sauti nzuri na mahadhi ya kuvutia ambayo yaliwavutia mno wote waliohudhuria. Hapa chini ni kipande cha video cha sehemu moja ya qiraa yake hiyo.

(Visited 167 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!