Taasisi moja ya misaada ya nchini Uturuki imegawa misahafu 30 elfu nchini Djibouti kwa ajili ya kuwarahishia Waislamu wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kujifunza vizuri Kitabu hicho kitakatifu.

Shirika la habari la Anadolu limeripoti habari hiyo katika mtandao wake wa lugha ya Kiarabu na kuongeza kuwa, msaada huo umetolewa chini ya kaulimbiu isemayo: “Dunia inasoma Qur’ani.”

Msaada huo ambao umetokea Izmir Uturuki kwa ajili ya Waislamu wa Djibouti umetolewa taasisi ya misaada inayoitwa Hayrat.

Ali Osman Aslanci, mwakilishi wa taasisi ya misaada ya Hayrat huko Izmir amewambia wandishi wa habari kwamba msaada huo umetolewa kama sehemu ya kuwa pamoja na watu wanaohitajia misaada barani Afrika.

Amesema, barani Afrika kuna watoto wengi Waislamu wanaolazimika kusoma Qur’ani kwenye loho za mbao na wanahitajia mno Misahafu. Amma kuhusiana na kazi za jumuiya ya misaada ya Hayrat ya Uturuki, Islanci amesema, hadi hivi sasa taasisi hiyo imeshagawa nakala laki 6 za Qur’ani Tukufu kwa Waislamu wa ndani ya Uturuki na nje ya nchi hiyo.

(Visited 89 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!