Waislamu nchini India wameilalamikia mahakama moja ya nchi hiyoi kwa kutupilia mbali ombi lao la kupuuza shauri la wanawake wa kibaniani la kutaka kuupora Msikiti wao. Ikumbukwe kuwa, kundi moja la wanawake wa Kihindu (kibaniani) limewasilisha ombi mahakamani, likitaka liruhusiwe kufanya sherehe zao za kibaniani ndani ya Msikiti mmoja nchini India.

Waislamu hao wa India wa mji wa Varanasi la jimbo la Uttar Pradesh, walikuwa wameiomba mahakama kutupilia mbali kesi na mabaniani hao waliodai kumiliki Msikiti wa Gyanvapi wa mji huo kwa madai ya eti kuwepo alama za mungu wao Msikitini humo. Lakini mahakama hiyo ya India imekataa ombi la Waislamu hao na kutangaza kwamba itasikiliza kesi hiyo. Mahakama hiyo pia imekubali kusikiliza shauri la mabaniani hao ambao wanaihesabu hatua hiyo ya mahakama kuwa ni ushindi mkubwa kwao.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, mahakama moja ya India imesema kuwa inachunguza madai yaliyowasilishwa na kundi la wanawake hao wa Kihindu wanaotaka kufanya sherehe zao za kibaniani ndani ya Msikiti katika moja ya miji yenye mabaniani wengi kaskazini mwa nchi hiyo.

Madai hayo yanaweza kuwa sababu ya kuzuka ugomvi mwingine mkubwa wa kidini kati ya Wahindu walio wengi na Waislamu walio wachache, ambao ni takriban watu milioni 200 kote nchini India. Ikumbukwe kuwa, Msikiti huu uko katika eneo lenye wafuasi wengine wa Waziri Mkuu Narendra Modi ambaye hafichi hata kidogo chuki zake dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Bloomberg, makundi ya kibaniani yametangaza kuwa eti kuna alama zinazohusiana na mungu wao “Shiva” ndani ya Msikiti huo. Viongozi wa Kiislamu wanakanusha suala hili na kuitaka mahakama isikubali madai ya mabaniani hao ili kuepusha umwagaji mwingine wa damu.

Msikiti wa Gyanvapi upo katika mji wa Varanasi, kando ya Mto Ganges, ambao ni mtakatifu kwa Wahindu.

Vishnu Shankar Jan, wakili wa kundi la wanawake hao wa kibaniani aliwaambia waandishi wa habari kwamba mahakama siku ya Jumatatu iliamua kuendelea kusikiliza shauri lao.

Mahakama hiyo imepanga kusikiliza shauri hiyioi Septemba 22 2022 ili kujadili iwapo mabaniani wanaweza kuruhusiwa kuingia Msikitini huo kuenesha hafla na ibada zao au la.

Serikali ya kibaniani inayoongozwa na Waziri Mkuu Narendra Modi inaonesha wazi kuchochea mashambulizi dhidi ya Waislamu wa India mashambulio ambayo yameongezeka kwa namna mbalimbali hivi sasa.

(Visited 69 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!